"Kazi" ya kwanza kabisa ya Jumuiya ya Sant'Egidio ni sala. Kwa kusoma maandiko matakatifu vijana hao walipata changamoto ya kuishi maisha yao kikamilifu zaidi: waligundua mwito wa kuwa wafuasi, mwito ambao Yesu aliutangaza kwa vizazi vyote. Ni mwito wa kubadilisha maisha, kuacha kuishi kwa ajili ya mtu binafsi na kuanza kwa hiari kuwa chombo cha upendo mkubwa zaidi kwa watu wote, wanaume kwa wanawake, na hasa wale walio maskini zaidi. Kuishi na kusikiliza Neno la Mungu kama jambo la umuhimu zaidi katika maisha ina maana ya mtu kukubali kumfuata Yesu badala ya kufuata njia zake binafsi.
Mfano halisi zaidi ni ile Jumuiya inayosali, iliyokusanyika pamoja kusikiliza Neno la Mungu. Ni kama ile familia ya wanafunzi waliomzunguka Yesu. Kuungana na kudumu katika sala (Matendo 2:42) ndiyo njia nyenyekevu inayokabidhiwa kama mfano na jukumu kwa wanachama wote wa Jumuiya ya Sant’Egidio. Sala ndiyo njia kuu ya kujiweka karibu na maneno ya Yesu na sala yake mwenyewe, na hata sala za vizazi vilivyopita, kwa mfano Zaburi, katika kuwasilisha kwa Bwana mahitaji ya watu maskini, mahitaji yetu wenyewe, na mahitaji ya ulimwengu nzima.
Hii ndiyo maana, kule Roma, na katika miji mingine nchini Italia, Ulaya na kote duniani, Jumuiya zote hukusanyika mara nyingi iwezekanavyo kusali. Katika miji mingi kuna sala za pamoja ambazo ni wazi kwa kila mtu. Kila mwanachama wa Jumuiya anahitajika kujiwekea nafasi kwa ajili ya sala ya binafsi na kusoma Neno la Mungu peke yake katika maisha yake, akianzia na Injili.
|
Personal prayer
|